KUTOKA 6 ;6-7 6 Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa; 7 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri. MATHAYO 15;30-31 30 Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya; 31 hata ule mkutano wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.
KWA HESHIMA NA SHUKRANI KWA MUNGU, FAMILIA YA BW. NA BIBI PAUL MBIWI OROTA WA UCHAU KIBOSHO, WANAYO FURAHA KUKUJULISHA/KUWAJULISHA KUWA KIJANA WAO MPENDWA SHEMASI JOSEPHAT MSAKURE OROTA ANATARAJIA KUPEWA DARAJA TAKATIFU LA UPADRI TAR 06.07.2017. HIVYO UKIWA KAMA NDUGU WA KARIBU WA FAMILIA HII UNAOMBWA KUSHIRIKIANA NAO KATIKA MAANDALIZI YA KUFANIKISHA SHEREHE HII MUHIMU YA UPADRISHO NA MISA YAKE YA SHUKRANI. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA DADA YAKE, RENALDA OROTA 0756 315 726