UTANGULIZI
Kikundi cha UMOJA
WA VIJANA WA UKOO WA OROTA (UVUO) kimeazishwa rasmi Oktoba 2016, kikundi hiki si
cha kibiashara na kimeundwa kwa mudhumuni ya kuwaleta pamoja Vijana wa Ukoo wa
Orota ili kudumisha UNDUGU NA MSHIKAMANO
wetu na kukua kama familia moja yenye kupendana na kumcha Mungu.
Taratibu za
kikundi hiki cha UVUO zimeandikwa
katika katiba hii na ndizo zitakazotumika kama mwongozo wa kikundi katika mambo
yote yahusuyo uendeshaji wa kikundi.
Katiba hii
imepitishwa kwa kauli moja na wanachama waanzilishi na kila mwanachama
atakayejiunga na kikundi atawajibika kuisoma katiba hii, kuielewa na kuitetea.
1.
TARATIBU ZA
KIKUNDI
1.1.
JINA LA
KIKUNDI NA MAKAO MAKUU
(a)
Jina la
Kikundi litakuwa “UMOJA WA VIJANA WA
UKOO WA OROTA” (UVUO)
(b)
Makao makuu
ya Kikundi yapo Moshi, Kilimanjaro..
( c)
Muhuri wa
Kikundi utakuwa na maneno UVUO
1.2.
MADHUMUNI
(a)
Kuwaunganisha pamoja Vijana wa
Ukoo wa Orota kutoka mashinani hadi mijin.
(b) Kuwaleta
pamoja Vijana wa Ukoo wa Orota ili kufahamiana na kuweza kuendeleza desturi na
mila nzuri za Ukoo wa Orota ikiwa ni pamoja na kusaidiana wakati wa shida na
raha.
(c) Kuanzisha
mfuko wa UVUO ambao unaweza kusaidia
katika maendeleo ya familia zetu hasa katika swala zima la elimu, tafrija,
mazishi na ujasiriamali kuendana na kanuni za katiba.
(d) Kuanzisha
miradi ya maendeleo yenye lengo la kuhakisha kikundi kina uwezo wa kutekeleza
shughuli zake.
2. UANACHAMA
(b)
Mtu yeyote mwenye umri wa kuanzia
miaka 18 na kuendelea anaweza kuomba uanachama katika kikundi hiki iwapo anazo
sifa stahili za kujuinga na kikundi kama zilivyoainishwa katika katiba hii.
(c)
Wanachama washiriki watachaguliwa
na kufanywa wanachama baada ya kujaza fomu maalum ya maombi, na maombi yao
kupendekezwa na wanachama waanzilishi wasiopoungua wawili.
(d)
Kwamba maombi yote ya kujiunga na
kikundi yatajadiliwa katika Mkutano Mkuu (au mkutano wa wanachama ulioitishwa
kwa ajili hiyo) wa kikundi, na yatakubaliwa kwa kura. Ili mtu aweze kuwa
mwanachama atatakiwa kukubaliwa na wanachama wasiopungua asilimia hamsini katika mkutano halali wa kikundi.
(e)
Sifa za
Uanachama
(i)
Isipokuwa kwa wanachama
waanzilishi wa kikundi hiki ambao kwa kutia saini katiba hii tayari wanafahamu
malengo ya kikundi hiki, mtu yeyote mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea
ambaye Ukoo wake ni OROTA na
aliyesoma na kuelewa katiba hii anaweza kuomba kuwa mwanachama wa Kikundi hiki.
(ii)
Mwanachama anatakiwa kuwa tayari
kufanya kazi za kikundi kwa kujitolea na kuhakikisha kuwa anakuwa wa mchango
mkubwa katika kukamilisha madhumuni ya kikundi hiki.
2.1.
MASHARTI YA UANACHAMA
(a) Kiingilio: Ili kuwa
mwanachama kila mwanachama aliyepitishwa na Mkutano anapaswa kulipa kiasi cha
shilingi 10,000/=. Kiasi hiki cha
fedha chaweza kulipwa kwa mkupuo mmoja au kwa awamu ndani ya miezi mitatu ya
kwanza.
(b) Ada: kila
mwanachama anapaswa kulipa ada ya kila mwezi kiasi cha shilingi 3,000/= (36,000/= kwa Mwaka). Mwanachama atakayeshindwa kulipa ada ya mwezi
kwa miezi mitatu mfululizo atakuwa amejivua uanachama na iwapo atataka kurudi
itambidi alipe faini ya shilingi 20,000/=
pamoja na malimbikizo ya miezi yote mitatu.
(c) Malipo yote
yatafanywa kwa Mweka Hazina na atatakiwa kutoa risiti kwa kila malipo
atakayopokea.
(d) Mweka hazina
atawajibika kuweka fedha katika acunt ya bank kwaajili ya kikundi.
(e) Kila
anayetaka kujiunga na kikundi ni lazima apewe nakala ya katiba ambayo ataisoma
na akikubaliana na taratibu zote itabidi asaini fomu maalum kama ushahidi kuwa
anakubaliana na masharti yote ya kikundi na yuko tayari kuwa mwanachama.
2.2.
HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA
(a) Kila
mwanachana ana haki ya kutoa mawazo yake bila woga hata kama mawazo hayo
yatapingana na kiongozi yoyote au mwanachama mwingine.
(b) Kila
mwanachama ana haki ya kupiga kura kuchagua viongozi au kugombea nafasi yoyote
ya uongozi kwa mujibu wa katiba.
(c) Kila
mwanachama ana wajibika kuhudhuria katika shughuli zote zinazohusu kikundi na
wanachama wenzake bila ubaguzi.
(d) Kila
mwanachama ana wajibu wa kusoma na kuielewa vyema katiba ya Kikundi na kufuata
maelekezo yake. Atakayekwenda kinyume kwa makusudi atahesabiwa kuwa ni msaliti wa kikundi na
hatua dhidi yake zitachukuliwa ikiwepo kupewa onyo au kufukuzwa uanachama.
2.3.
KUPOTEZA UANACHAMA
Mwanachama anapoteza haki yake ya
kuwa mwanachama kutokana na sababu zifuatazo:
(i)
Kifo
(ii)
Kutohudhuria vikao vya kikundi
bila taarifa yoyote kwa MIAKA MITATU mfululizo au kubainika kuwa sababu
zinazotolewa na kutohudhuria vikao siyo za msingi.
(iii)
Kushindwa kutimiza masharti ya
katiba,
(iv)
Kujiuzulu
(v)
Kutowakilisha michango ya mwezi
kwa miezi mitatu mfululizo.
(vi)
Ikidhibitika kwamba mwanachama
ana tabia za uchochezi zinazovuruga amani baina ya wanachama.
(vii)
Kufanya kazi binafsi kwa kutumia
jina la kikundi bila kikundi kuwa na taarifa.
(viii) Ikiwa
italetwa mada na mwanachama/ kikundi ya kumfukuza mwanachama uanachama kwa
sababu ya kushindwa kutimiza masharti ya katiba au uchochezi. Mleta mada
atatakiwa kupeleka kwa maandishi sababu za mada yake na mwanachama
anayetuhumiwa atapewa nafasi ya utetetezi wa maandishi. Maumuzi yote yatatakiwa
kufanywa katika mkutano mkuu kwa kura zisizopungua theLuthi mbili ya wanachama
waliohudhuria.
(ix)
Endapo mwanachama atapoteza haki
yake ya uanachama, kiingilio na michango
aliyotoa havitarudishwa.
3. VIONGOZI
3.1.
KAMATI KUU
Kikundi kitakuwa na viongozi wa kamati kuu
wafuatao:
(a) Mwenyekiti;
Josephat Orota
(b) Makamu
Mwenyekiti; Renalda Orota
(c) Katibu;
Agnes Patrick Orota
(d) Katibu
Msaidizi; Joseph Remi Orota
(e) Mweka
Hazina: Agnes Martini Orota (mweka sahihi bank)
(f) Mweka Hazina
Msaidizi
3.2.
KAMATI YA
NIDHAMU (NA MATUKIO)
Kikundi pia kitakuwa na
viongozi wa kamati ya Nidhamu na Matukio ambao ni:
(a) Mwenyekiti:
Josephat Orota
(b) Makamu
Mwenyekiti: Renalda Orota
(c) Katibu: Agnes Patrick Orota
(d) Katibu msaidizi: Joseph Remi Orota
(e) Pascal Orota
(f) Rose Patrick Orota (Mweka sahihi bank)
(g) Cosmas Peter Orota
(h) Leon Orota
(i) Rodrigers Orota
v Nafasi za uongozi zilizotajwa hapo juu zitajazwa
kwa wagombea kuchaguliwa na wanachama kwenye mkutano mkuu utakaohudhuriwa na
theluthi mbili ya wanachama hai.
v Kipindi cha uongozi kitakuwa cha muda wa MIAKA MIWILI mpaka hapo itakapoamuliwa
vingine.
v Uchaguzi mdogo unaweza kufanyika iwapo kiongozi
atapoteza haki yake ya kuwa mwanachama.
v Ili mwanachama aweze kugombea au kuchaguliwa
kushika nafasi yoyote ya uongozi ni lazima awe amemaliza kulipa kiingilio na
ada na amedumu ndani ya chama kwa kipindi kisichopungua mwaka Mmoja ili awe amefahamika vizuri na wanachama
wengine.
4.
VIKAO
v Mambo yafuatayo
yatazingatiwa kuhusu vikao.
4.1.
AINA ZA
VIKAO
v Kikundi kitakuwa na vikao vya aina tatu;
(i)
Kikao cha
kila mwezi ambacho kitajadili maendeleo ya kikundi, kuidhinisha wanachama wapya
na kupeana taarifa ya mambo mbalimbali katika kujiendeleza. Kikao hiki
kitafanyika kila JUMAPILI ya mwanzo wa mwezi saa kumi na moja jioni (11:00) kwa
njia ya mtandao wa WHATSAPP.
(ii)
Vikao vya
kila wiki kwa viongozi wote wa kikundi kujadili namna ya uongozi bora wa
kikundi changamoto mbalimbali za wanachama.
(iii)
Mkutano mkuu
ambao utafanyika kila baada ya mwaka mmoja. Kikao hiki kitaangalia mafanikio na
matatizo na ndicho kitahusika na uchaguzi wa viongozi pale viongozi wanapokuwa
wamemaliza muda wao. Kikao hiki lazima kihudhuriwe na wanachama wasiopungua
theluthi mbili ya wanachama hai. Wanachama hai ni wale waliolipia vizuri ada
zao na wanaohudhuria mikutano/vikao vya kikundi.
(iv)
Kikao cha
dharura ambacho kitaitishwa na katibu wa kamati ya nidhamu na matukio na
kuendeshwa na mwenyekiti wa kamati ya nidhamu na matukio.
4.2.
TARATIBU ZA VIKAO
(i)
Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti
ndiye atakayeendesha vikao akisaidiana na Katibu atakayechukua kumbukumbu zote
za vikao.
(ii)
Kiongozi yoyote anayo wajibu
wakumbusha au kumuuliza katibu mda wa kikao.
(iii)
Kikao kitajadili mada
zitakazowasilishwa na ikiwa kutatokea mvutano, basi kura ya siri/wazi itatoa
uamuzi na kama baada ya kupiga kura matokeo yatakuwa sawa uamuzi utatolewa na
mwenyekiti kwa kupiga kura ya turufu.
(iv)
Maamuzi yatakayoamuliwa na
theluthi mbili ya wanachama yamepitishwa.
(v)
Mwanachama ambaye hatahudhuria
kikao kwa sababu yoyote ile anatakiwa kutoa taarifa kwa katibu. Udhuru uwe kwa
maana halisi ya udhuru na siyo kwa nia ya kukwepa kikao.
5. FEDHA ZA KIKUNDI
Katika maswala ya fedha kutakuwa na taratibu kwa
upande wa makusanyo (mapato) na matumizi ya fedha za mapato. Taratibu hizi
zitakubaliwa katika Mkutano Mkuu wa Kikundi.
5.1.
MAPATO
Mapato ya kikundi yatatokana
na;
(a)
michango ya
wanachama itakayotolewa kama kiingilio, ada ya mwezi na michango mbalimbali
kutoka kwa wanachama pale inapobidi.
(b) Misaada kutoka kwa wahisani na wafadhili. (ndani
na nje ya nchi)
(c)
Miradi
mbalimbali itakayobuniwa na wanachama katika kuhakikisha kuna ustawi wa kikundi
kwa ajili ya kutekeleza madhumuni ya kikundi.
5.2.
MATUMIZI YA MAPATO
(a) Mapato yote
ya kikundi yatatumika kwa ajili ya kutekeleza madhumuni ya kikundi.
(b) Kikundi
kitatumia mapato yake kwa ajili ya kusaidia wanachama pamoja na kuchangia
misiba au sherehe kwa wanachama wake.
(c) Hakutakuwa
na mikopo kutoka kwenye mfuko wa kikundi na fedha za kikundi zitatumika kwaajili
ya kusaiaidia wanachama kama ilivyo ainishwa hapo juu (ab).
6. MENGINEYO
(a)
Wanachama katika Mkutano Mkuu wanaweza
kuamua kwa kura zisizopungua asilimia tisini (90%) wa wanachama hai
walioshiriki kufanya marekebisho ya katiba hii. Taarifa ya marekebisho na aina
ya marekebisho lazima itolewa na Mwenyekiti kwa wanachama hai wote siku
thelathini (30) kabla ya kikao kinachotarajiwa kujadili marekebisho ya Katiba.
(b) Mkutano Mkuu
wa kikundi waweza kuamua kusitisha shughuli za Kikundi hiki kwa kura
zisizopungua asilimia tisini (90%) za wanachama hai. Taarifa ya chini ya
kifungu hiki lazima itolewe na Mwenyekiti kwa wanachama hai wote siku
thelathini (30) kabla ya kikao. Iwapo Huduma ya Kikundi hiki itasitishwa basi
mali zote za kikundi zitahamishiwa kwa kikundi cha UKOO WA OROTA.
(c)
Mali zote za Kikundi zitakuwa
chini ya jina la kikundi na zitakuwa chini ya uongozi wa Kikundi ambao muda
wote utatunza kumbukumbu za mali zinazomilikiwa na kikundi.
(d) Katika
upanuzi wa shughuli zake, kwa makubaliano katika Mkutano Mkuu, kikundi chaweza
kujisajilii chini ya sheria yoyote husika ili kuleta ufanisi katika kutekeleza
madhumuni yake.
(e)
Mwanachama yoyote mwenye
malalamiko katika utekelezaji wa shughuli za Kikundi aweza kuyawasilisha kwa
Mwenyekiti ambaye atayafikisha katika Kamati Kuu ambayo itayajadili na
kutayatolea ufafanuzi.
Hongereni kwa katiba nzuri ndg zanguni akina Orota wa kibosho
ReplyDeleteWakuu mko vizur pia asante kwakunipa somo maana nimepewa jukumu la kuandaa kama hiyo pia .
ReplyDeletehongera sana
ReplyDeleteMmenipa torch , nmepata ABC
ReplyDeleteCongratulations Orota Family Kwa katiba nzuri
ReplyDeleteVizuri sana orota family
ReplyDelete